Sunday, February 10, 2013

NATO AFGHANISTAN YAPATA MKUU MPYA

Jenerali Joseph Dunford wa jeshi la Marekani amechukua nafasi ya mkuu wa majeshi ya kulinda amani ya jumuiya ya kujihami ya NATO nchini Afghanistan hii leo kutoka kwa Jenerali John Allen aliyekuwa akiongoza hapo awali. Mabadiliko hayo yanafanyika wakati huu ambapo majeshi ya NATO yakijiandaa kuondoka Afghanistan ifikapo mwaka 2014. Dunford huenda akawa kamanda wa mwisho katika vita hivyo vya Marekani dhidi ya makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali, atakayekuwa na jukumu la kuyarejesha nyumbani majeshi yao baada ya kipindi cha zaidi ya miaka 11. Jenerali huyo atasimamia pia mpango wa kukabidhi jukumu

 la ulinzi wa Afghanistan mikononi mwa Waafghan wenyewe. Licha ya kuendelea kwa mashambulizi ya umwagaji damu ya Kundi la Taliban dhidi ya serikali ya Rais Hamid Karzai na majeshi ya NATO, Allen ambaye anaacha wadhifa huo ili kuwa kuwa Kamanda mkuu wa NATO katika Ulaya, amesema kuwa wako njiani kuelekea ushindi. Shughuli za kukabidhi uongozi zimefanyika katika makao makuu ya Shirika la NATO katika mji mkuu wa Afganistan, Kabul. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO