Jumuiya za Kiislamu zinazidi kutambuliwa rasmi nchini Ujerumani kiasi kwamba dini ya Kiislamu imekuwa sehemu ya jamii ya nchi hiyo. Ayrvl Barrels, Msemaji wa Baraza la Uratibu la Waislamu wa Ujerumani amesema kuwa jimbo la Bremen siku kadhaa zilizopita lilizitambua rasmi jumuiya tatu za Kiislamu na inatarajiwa kuwa jumuiya nyingine kama hizo zitatambuliwa rasmi pia katika majimbo mengine ya Ujerumani. Barrels ameongeza kuwa kutambuliwa rasmi jumuiya hizo tatu mpya za Kiislamu katika jimbo moja ni dhihirisho kwamba Uislamu umekuwa sehemu ya jamii ya Ujerumani. Ayrvl Barrels amesema Bremen ni jimbo la tatu huko Ujerumani kuzitambua rasmi jumuiya za Kiislamu nchini humo. Hii ni katika hali ambayo mwezi Disemba mwaka jana jimbo la Hessen huko Ujerumani pia lilizitambua rasmi taasisi mbili za Kiislamu kama taasisi za kidini ambazo zilikuwa na lengo la kutoa darsa za Kiislamu katika jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO