Korea Kaskazini imeitaarifu China kuwa iko tayari kufanya kwa uchache jaribio moja jingine la nyuklia mwaka huu kama sehemu ya juhudi zake ya kuilazimisha Washington ikubali mazungumzo ya kidiplomasia. Duru moja iliyokaribu na serikali za Beijing na Pyongyang imeeleza kuwa Pyongyang hivi karibuni itafanya jaribio la nne na la tano la nyuklia pamoja na roketi. Imeongeza kuwa majaribio hayo yatafanywa mwaka huu iwapo Marekani haitashiriki katika mazungumzo na Pyongyang na kutupilia mbali siasa zake za kutaka kubadilishwa utawala huko Korea ya Kaskazini. Itakumbukwa kuwa tarehe 12 Februari mwaka huu Pyongyang ilitangaza kuwa imefanya kwa mafanikio jaribio lake la tatu la nyuklia ambalo lilitekelezwa kwa umahiri mkubwa. Jaribio hilo lililaaniwa na Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na nchi kadhaa zikiwemo Marekani, Korea ya Kusini, Russia na Japan.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO