Maelfu ya wafuasi wa chama cha Kiislamu cha Sa'adat wamefanya maandamano makubwa mjini Istanbul wakipinga uwekaji wa makombora ya Patriot nchini Uturuki. Imedaiwa kuwa makobora hayo ni ya kulinda ardhi ya Uturuki. Waandamanaji hao waliojawa na hasira pia wamepinga vikali kuingia nchini humo askari wa kigeni kutoka nchi za Ulaya kwa minajili ya kusimamia makombora hayo. Aidha waandamanaji walichoma picha za makombora hayo huku wakitoa nara za kuilaani Marekani, madola ya Magharibi na serikali ya Uturuki ya Recep Tayyip Erdoğan Waziri Mkuu wa nchi hiyo. Wamesema kuwa, nchi za Ulaya zinaisukuma Uturuki kuingia katika mgogoro wa kivita na nchi za eneo suala linalopingwa vikali na wananchi wengi wa nchi hiyo. Wameongeza kwa kusema kuwa, hatua ya Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO ya kuweka kambi 28 za kijeshi katika ardhi za Uturuki na kuweka makombora ya Patriot ni hatua iliyowazi ya uvamizi wa shirika hilo nchini Uturuki.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO