Serikali ya Nigeria imesema kuwa ipo tayari kuangalia pendekezo lililotolewa na kundi la Boko Haram la kusitisha mapigano. Makamu wa Rais wa Nigeria Namadi Sambo amesema, Abuja inakaribisha pendekezo hilo la usitishaji mapigano la Boko Haram na kwamba serikali itajitahidi kuhakikisha kwamba amani inapatikana nchini humo. Sambo amesema hayo alipotembelea mji wa kusini mashariki mwa Nigeria wa Maiduguru ambao unahesabiwa kuwa ngome ya wapiganaji wa Boko Haram. Hii ni mara ya kwanza mji huo kutembelewa na Makamu wa Rais tangu mwaka 2009.
Kundi lililofurutu ada la Boko Haram limehusika katika milipuko na mashambulizi tofati katika miji kadhaa ya Nigeria tangu mwaka 2009. Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa, zaidi ya watu 1000 wameuawa kutokana na mashambulizi ya kundi hilo kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka uliopita wa 2012.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO