Monday, February 04, 2013

MAREKANI YAIPATIA CAIRO NDEGE ZA KIVITA


Marekani imeipatia Misri ndege nne za kivita aina ya F-16 kama sehemu ya msaada wa kijeshi wa kila wa mwaka wa Washington kwa nchi hiyo.

Hatua hiyo imetajwa na Wazir wa Ulinzi wa Misri Abdulfattah al Sisi kuwa ni ushirikiano wa kijeshi unaoimarika kati ya Cairo na Washington. Maafisa wa serikali ya Marekani na Misri wamefanya sherehe hii leo katika kuadhimisha kuwasili kwa ndege hizo. Hata hivyo msaada wa huo wa ndege za kivita wa Marekani kwa Misri umekosolewa ndani ya Kongress ya Marekani baada ya Seneta wa Kentucky Ran Paul kuitaja hatua hiyo kuwa ni kosa kubwa. 
Ndege hizo za kijeshi ni sehemu ya jumla ya ndege 20 ambazo Washington ina mpango wa kuipatia Misri mwaka huu ambapo nne kati ya hizo tayari zimewasili nchini humo mwezi Januari mwaka huu na zingine zinatazamiwa kuwasili huko Misri baadae mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO