Monday, February 04, 2013

ERDOGAN ALAANI SHAMBULIO LA ISRAEL HUKO SYRIA


Waziri Mkuu wa Uturuki amelaani vikali shambulio la hivi karibuni la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kituo cha utafiti cha masuala ya sayansi nchini Syria. Recep Tayyip Erdogan amewaambia waandishi wa habari mjini Istanbul kwamba, wale ambao wameidekeza Israel wanapaswa kutaraji hatua kama hiyo ikifanywa na Israel wakati wowote.
Waziri Mkuu wa Uturuki amesema kama ninavvyomnukuu, "kama ambavyo nimekuwa nikisema siku zote ninakariri tena kwamba, Israel ina fikra ya kueneza ugaidi. Aidha Erdogan amesema, suala la kukiuka anga ya nchi nyingine halikubaliki na bila shaka kile kilichofanywa na Israel ni kitu ambacho kinakinzana kikamilifu na sheria za kimataifa na kwamba kuna haja ya kuchukuliwa hatua zaidi ya kulaani. Hayo yanajiri katika hali ambayo, hatua ya Israel ya kukiuka anga na mamlaka ya Syria na kushambulia kituo cha utafiti wa masuala ya sayansi imeendelea kulaaniwa vikali na duru za kieneo na kimataifa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO