Wednesday, February 13, 2013
MIKE GRAVEL: MAREKANI INAJIFANYA POLISI WA ULIMWENGU
Seneta wa zamani wa Marekani amesema kuwa Marekani inajifannya polisi wa dunia jambo ambalo litaitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro mkubwa ambao haijawahi kuushuhudia. Mike Gravel seneta wa zamani wa Marekani amesema kuwa Washington imepoteza uwezo wa kushiriki kwa uadilifu katika masuala yanayoihusu dunia baada ya kushutumiwa na kukosolewa vikali kimataifa siasa zake za nje za ukandamizaji hususan zile zinazohusiana na mpango wake haramu wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani. Gravel ameitahadharisha Marekani kwa kile alichokitaja kuwa kitakuja kuithibitishia nchi hiyo kuwa mgogoro mkubwa dhidi yake kutokana na hatua yake ya kujichukulia sheria mkononi na kuua watu ovyo katika pembe mbalimbali za dunia. Amesema Marekani inapaswa kuondoa vikosi vyake vilivyoko katika nchi mbalimbali duniani na kuwaacha raia wa nchi hizo watatue matatizo yao wenyewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO