Friday, February 08, 2013

ICC YAITAKA LIBYA IMKABIDHI SENUSSI

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imeitaka serikali ya Libya imkabidhi mkuu wa zamani wa vyombo vya ujasusi vya nchi hiyo Abdullah al-Senussi kwa mahakama hiyo yenye makao yake nchini Uholanzi.
Mahakama ya ICC ilitangaza jana kuwa serikali ya Libya inapasa kumkabidhi Abdullah al-Senussi kwa mahakama hiyo haraka iwezekanavyo. Taarifa ya ICC imesema kuwa iwapo Libya itakataa kumkabidhi Al Senussi, mahakama hiyo italiomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lichukue hatua katika uwanja huo. Libya inasema mwana wa dikteta wa zamani wa nchi hiyo Saiful Islam Gaddafi na mkuu wa vyombo vyake vya ujasusi Abdullah Al Senussi wanapaswa kuhukumiwa katika ardhi ya nchi hiyo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka mahakama ya ICC ifanye uchunguzi kuhusu mapinduzi ya mwaka 2011 nchini Libya

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO