Naibu Mwenyekiti wa baraza la utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesesema kuwa nguvu ya sasa ya muqawama katika eneo imefikia kiwango cha hali ya juu. Sheikh Nabil Farooq amesema baada ya kusimama kidete kwa miaka 30 mbele ya utawala wa ghasibu wa Kizayuni, leo hii nguvu ya muqawama katika eneo imefikia kiwango cha juu kabisa. Naibu Mwenyekiti wa baraza la utendaji la harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa utawala wa Kizayuni ambao umezishambulia Sudan, Ukanda wa Ghaza na Syria na kutumia vibaya hali ya mgogoro katika maeneo hayo hivi sasa hauna uthubutu wa kuishambulia Lebanon kwa sababu hauwezi kuvumilia mlingano na mashambulio ya kushtukiza ya muqawama wa Lebanon. Sheikh Farooq amesema lengo la maadui kuzusha machafuko huko Syria liko wazi kikamilifu na kama ambavyo Hizbullah ilivyowahi kusema huko nyuma ni kuwa maadui wameazimia kwa dhati kuindoa Syria katika mhimili wa muqawama katika eneo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO