Tuesday, February 12, 2013

LEVROV ASEMA UFARANSA INAVUNA ILICHOKIPANDA LIBYA

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amekosoa siasa za Ufaransa na kubainisha kwamba, vita vya Paris huko Mali ni natija ya hatua zake za kuyapatia silaha makundi yanayobeba silaha ya nchini Libya. Sergey Lavrov amesema, hivi sasa Ufaransa inavuna ilichopanda; kwani makundi ambayo leo yanapigana na Paris kaskazini mwa Mali ndio yale yale ambayo Ufaransa iliyopataia silaha ili yaendeshe vita dhidi ya kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.  Ameongeza kuwa, hii leo kuna makundi mengine ya wabeba silaha ya Libya ambayo yanaendesha vita dhidi ya Rais Bashar al-Assad wa Syria na ambayo pia huko nyuma yalipatiwa silaha za Ufaransa ili yaiangushe serikali ya Kanali Muammar Gaddafi wa Libya.  Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema kama ninavyomnukuu: Ni jambo la kushangaza kuwa, washirika wetu huko Magharibi hawadiriki jambo hili. Mwisho wa kunukuu. Wakati huo huo, Alexei Doulyan, balozi wa Russia nchini Mali amesema kuwa, mapigano ya sasa kaskazini mwa nchi hiyo ni muendelezo wa mgogoro wa Libya.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO