Wanajeshi wa Ufaransa na Tchad wananedelea na operesheni hiyo kwa sasa a inawalenga wapiganaji wa kiislam waliotawanyika katika milima ya Adrar na Ifoghas mbali zaidi kaskazini mashariki mwa Mali na inaweza kuendelea hadi mjini Tessalit
Wanajeshi hao wa Tchad na Ufaransa walitembea kutoka Kidal hadi Aguelhok kwenye umbali wa kilometa 160 na mji wa Kidal, ni eneo lenye milima ambako linasadikiwa huenda ndiko waliko jificha wapiganaji wa kiislam, kwa sasa hakuna mapambano
Wanajeshi hao wanampango wa kuendelea hadi mjini Tessalit kwenue umbali wa kilometa zisizofikia 100 ambako kuna uwezekana mji huo nao ukaanguka mikononi mwa majeshi hayo.
Operesheni hiyo imefanikiwa kupambana na wanamgambo wa kiislamu waliokuwa wakishikilia eneo la kaskazini na kutishia kuudhibiti mji mkuu wa Mali, Bamako.
Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imesema kuwa Operesheni ya katika koloni lake la zamani imegharimu Euro milioni 70.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO