Sunday, February 10, 2013

SUDAN YAONYA KUACHA MASHAMBULIZI YA ANGA


Serikali ya Marekani imeitaka Sudan kuacha kufanya mashambulizi ya anga huko Darfur huku ikiwataka wataalamu wa vikwazo kutoka Umoja wa mataifa kuruhusiwa kufanya uchunguzi kwa mapana nchini humo.Msemaji wa serikali ya Marekani Victoria Nuland amesema kuwa shinikizo la kimataifa juu ya Sudan linaongezeka wakati uhasama katika majimbo ya Kordofan na Blue Nile dhidi ya waasi huko Darfur ikiongeza mvutano na jirani yao Sudan Kusini.

Mara kwa mara Umoja wa mataifa umelalamika kufuatia ugumu wa kuyafikia maeneo yenye mgogoro huko Darfur na kusema kuwa maeneo hayo yamezuiliwa huku ripoti zikiarifu kumekuwepo mashabulizi ya anga yanayofanywa na vikosi vya serikali. Kujirudia kwa mapigano kumelazimisha maelfu ya raia wa Sudan kuyahama makazi yao ili kuyasalimisha maisha yao.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO