Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana lilitoa tamko kali la kulaani
hatua ya Korea Kaskazini ya kufanyia majaribio silaha za nyuklia na kusisitiza
kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya Pyongyang. Balozi wa Kudumu wa Marekani
katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice amesema nchi yake inalichukulia suala hilo
kwa uzito mkubwa. Hata hivyo nchi 15 wanachama wa baraza hilo hazikuafikiana juu
ya hatua zipi zichukuliwe dhidi ya Korea Kaskazini. China ambayo ni mshirika wa
karibu wa kibiashara wa Pyongyang imepinga wazo la kutumiwa nguvu za kijeshi na
imetaka vikwazo zaidi viwekwe kama njia ya kuibana zaidi Korea Kaskazini. Kwa
upande wake, Pyongyang imetishia kwamba itafanya majaribio mengine mawili ya
silaha zake za nyuklia; jambo linalotarajiwa kuzusha wasiwasi mkubwa katika nchi
jirani ya Korea Kusini.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO