Rais Barack Obama wa Marekani amekiri kwamba nguvu za kijeshi na kiuchumi za
nchi yake zinaendelea kupungua siku baada ya siku na kwa msingi huo ameahidi
kuondoa wanajeshi 34 000 nchini Afghanistan mwanzoni mwa mwaka ujao. Pia amesema
vita vinavyoongozwa na nchi yake huko Afghanistan vitafikia kikomo mwishoni mwa
mwaka ujao. Akizungumza kwenye hotuba muhimu kwa taifa usiku wa kuamkia jana,
Obama amesema matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Marekani kwa sasa ndio sababu
kubwa ya kupungua nguvu na satua ya nchi hiyo duniani. Amesema kipindi chake cha
pili cha uongozi kitatoa kipaumbele kwa masuala ya kiuchumi na jinsi ya
kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira. Hotuba hiyo hutolewa mara moja kila
mwaka mbele ya wajumbe wa Kongres na Rais Obama hakusita kuendeleza matamshi ya
kijuba ya Marekani kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Syria na nchi zingine
zinazopigania haki duniani. Kuhusu Syria kiongozi huyo amesema kuwa, Washington
itaendeleza mashinikizo dhidi ya Rais Bashar Asad sambamba na kuendelea kuwaunga
mkono wapinzani wanaotaka kuipindua serikali halali ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO