Haki za Waislamu nchini Uingereza zimeendelea
kukiukwa huku wafungwa wa Kiislamu wanaotumikia vifungo katika magereza ya nchi
hiyo wakilazimishwa kula nyama ya nguruwe. Shirika moja la kutetea haki za
binadamu limetangaza kuwa, serikali ya Uingereza imekuwa ikikiuka haki za
wafungwa wa Kiislamu katika magereza ya nchi hiyo. Taarifa zaidi zinasema,
serikali ya Uingereza imekataa kupeleka nyama halali kwa ajili ya wafungwa wa
Kiislamu katika magereza ya nchi hiyo na badala yake imekuwa ikiwalazimisha
wafungwa hao wa Kiislamu kula nyama ya nguruwe ambayo kwa mujibu wa mafundisho
ya dini yao ni haramu. Imeelezwa kuwa, katika baadhi ya magereza wahusika
katika magereza hayo wamekuwa wakipeleka nyama ya nguruwe na kupuuza kwamba,
kuna wafungwa ambao ni wafuasi wa dini ya Kiislamu. Taarifa zaidi zinaeleza
kuwa, katika baadhi ya magereza nyama ya matumizi kwa ajili ya wafungwa
imepatikana ikiwa imechanganywa na nyama ya nguruwe. Shirika linalotetea
mageuzi katika magereza nchini Uingereza limetoa wito wa kufanyika uchunguzi
kuhusiana na ukiukaji wa haki za binadamu katika magereza ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO