Serikali
ya China imesisitiza kwamba, Iran ina haki kamili ya kunufaika na teknolojia ya
kisasa ya nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani. Hong Lei, Msemaji wa Wizara
ya Mashauri ya Kigeni ya China amesema kuwa, daima Beijing imekuwa ikiunga
mkono ushirikiano wa Tehran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki
(IAEA). Amesema, China inaamini kwamba, mazungumzo na ushirikiano ndio njia
pekee na sahihi ya kuondoa suutafahumu kuhusiana na suala la miradi ya nyuklia
ya Iran na imekuwa ikizishajiisha pande mbili hizo kushirikiana zaidi. Msemaji
huyo wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China ameongeza kuwa, Iran ikiwa
miongoni mwa nchi zilizotia saini Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa
Silaha za Nyuklia NPT ina haki ya kustafidi na teknolojia ya nyuklia kwa
matumizi ya amani. Licha ya kuwa miradi ya nyuklia ya Iran ni kwa ajili ya
matumini ya amani na imekuwa ikifanyika chini ya usimamizi wa Wakala wa
Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, lakini Marekani, utawala wa Kizayuni wa
Israel na waitifaki wao wamekuwa wakiituhumu Tehran kwamba, miradi yake ya
nyuklia ni kwa ajili ya malengo ya kijeshi, tuhuma ambazo hazina msingi wowote.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO