Jeshi la Marekani limetangaza kuwa, karibu wanajeshi 325 wa nchi hiyo walijiuwa mwaka 2012 na kiwango hicho ni kikubwa zaidi ikilinganishwa na idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouawa nchini Afghanistan mwaka 2012. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, wanajeshi 182 waliamua kujiuwa wakati wakiwa kwenye medani za vita na kesi zipatazo 130 zimeshathibitishwa na jeshi la Marekani, huku 52 zikiendelea kuchunguzwa. Jeshi la Marekani limeongeza kuwa, idadi ya wanajeshi wa nchi hiyo waliouawa nchini Afghanistan mwaka jana ilikuwa 312. Jenerali Howard Bromberg wa jeshi la Marekani amesema kuwa, idadi hiyo ya wanajeshi waliojiua mwaka jana ni kubwa mno katika historia ya jeshi la nchi hiyo. Utafiti mwengine umeeleza kuwa, karibu wanajeshi 22 wa zamani hujiuwa kila siku na idadi hiyo ni asilimia ishirini zaidi ya kiwango cha kujiuwa wanajeshi wa zamani wa nchi hiyo mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO