Wednesday, February 06, 2013

IRAN KUTUMA SATELAITI ANGA ZA MBALI


Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inapanga kutuma katika anga za mbali, satalaiti ijulikanayo kama Tolou (yaani mapambazuko).

Akizungumza na wataalamu wa anga za mbali hapa mjini Tehran, Vahidi amesema satalaiti ya Tolou itatumwa anga za juu kwa kutumia chombo cha kubeba satalaiti cha Simorgh. Satalaiti hiyo itarushwa  angani kutoka katika Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Imam Khomeini ambacho kimezinduliwa hivi karibuni hapa nchini Iran.
Vahidi ameongeza kuwa, baadhi ya nchi zilizoendelea duniani hadi hivi sasa hazina uwezo wa kutuma satalaiti katika anga za mbali na kwamba ni nchi tano tu duniani ambazo zina uwezo sawa na Iran katika uga wa satalaiti na anga za mbali. Januari 28 Iran ilituma nyani hai katika anga za mbali ambaye alirejea ardhini akiwa salama. Jamhuri ya Kiislamu ilitumia kombora la Kavoshgar Pishgam ambalo lilimpelekea nyani huyo umbali wa kilomita 120 angani. Iran ilirusha katika anga za mbali satalaiti ya kwanza iliyotengenezwa hapa nchini Iran ijulikanayo kwa jina la Omid (yaani Tumaini) mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO