Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amemwambia Rais Barack Obama wa Marekani aliyetembelea Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwamba hawatendelea na mazungumzo na Israel hadi ujenzi wa vitongoji utakaposimamishwa. Abbas alisema hayo baada ya Obama kuwataka Wapalestina waanze tena mazungumzo yanayoitwa eti ya kusaka amani na Israel. Obama pia amewataka Wapalestina eti waache kutaka kusimamishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Palestina, kama sharti la kuanza tena mazungumzo na Israel.
Wakati huo huo msemaji wa Harakati ya Mapamambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amesema, Rais Barack Obama wa Marekani amebainisha matakwa ya Wazayuni katika safari yake huko Ramallah. Sami Abu Zuhri amesisitiza kuwa, hotuba ya Obama haikuwa na kitu cha maana ndani yake. Ameongeza kuwa, Obama hakuwa na ahadi mpya kwa taifa la Palestina bali amesisitiza msimamo wa Marekani wa kutaka kuanza mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Wapalestina na Israel bila masharti yoyote, msimamo ambao ni ule ule wa Tel Aviv.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO