Friday, March 22, 2013

WATU KADHAA WAJERUHIWA KATIKA MRIPUKO SOMALIA

Duru za polisi ya Somalia zimeripoti kuwa, watu wengi wamejeruhiwa katika mlipuko wa kujitolea muhanga uliotokea hapo jana katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu. Taarifa zinasema kuwa, mtu mmoja alijilipua baada ya kushindwa kuingia katika kituo cha polisi kilichoko kwenye soko la Bakara mjini Mogadishu, ambalo huko nyuma lilikuwa ngome ya waasi wa as Shabab.
Katika upande mwingine Kamanda wa vikosi vya Umoja wa Afrika amesema kuwa, askari wa umoja huo wanawatayarisha askari wa Somalia kwa ajili ya kusimamia hali ya nchi hiyo iwapo vikosi vya Ethiopia vitaondoka nchini Somalia. Andrew Guti ambaye ni kamanda wa vikosi vya AMISOM ameashiria maeneo ya kusini magharibi mwa Somalia ambayo hadi sasa yanadhibitiwa na askari wa Ethiopia na kusema kwamba, wanatekeleza mipango itakayowawezesha askari wa Somalia kusimamia maeneo hayo baada ya kuondoka vikosi vya Ethiopia nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO