Mahakama moja nchini Italia leo imemhukumu Waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Silvio Berlusconi kifungo cha mwaka mmoja jela, kutokana na gazeti moja la familia yake kuchapisha taarifa iliovuja kwenye mtandao kuhusiana na kashfa moja ya Benki 2006. Hukumu hiyo hata hivyo inamaanisha kwamba Berlusconi tajiri mkubwa mwenye umri wa miaka 78 , hatotumikia kifungo hadi kwanza hatua ya kukata rufaa imemalizika, ambapo huenda mahakama kuu ikabatilisha hukumu hiyo. Pamoja na hayo kuhukumiwa kwa Berlusconi kumekuja katika wakati ambapo kuna utata wa kisiasa uliotokana na uchaguzi mkuu wiki iliopita, kukiwa hakuna chama kilichotokeza kuwa na wingi wa kuunda serikali peke yake.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO