Rais wa Senegal Macky Sall, ametoa wito wa kuimarishwa Madrasa za Kiislamu nchini humo. Sall anasema kuwa serikali itafunga Madrasa zote ambazo zitakosa kutimiza mahitaji ya usalama kwa watoto. Matamshi yake Rais Macky Sall, yanajiri baada ya watoto tisa kufariki kwenye ajali ya moto katika Madrasa moja iliyoko karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Dakar. Moto huo, ulizuka wakati watoto 45 wa kati ya umri wa miaka 6 na 12, wakiwa ndani ya chumba kimoja katika eneo la Medina. Inaarifiwa kuwa huenda mshumaa ndio uliosababisha ajali hiyo ya moto uliozuka mwanzoni mwa wiki hii. Baada ya kutembele eneo kulikotokea mkasa huo hapo jana, bwana Sall, amesema kuwa shule za mafunzo ya kidini ambazo zinawadhulumu watoto na kukosa kuhakikisha usalama wao, lazima zifungwe. Kumekuwa na tuhuma kwamba baadhi ya waalimu wa Madrasa hutumia shule hizo za kidini kujitajirisha.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO