Tony Blair, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, kwa mara nyingine tena amejitokeza na kutetea uamuzi wa kushambuliwa kijeshi Iraq, licha ya kupita miaka kumi tangu vikosi vamizi vya Marekani na Uingereza viivamie na kuikalia kwa mabavu Iraq. Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza ametetea hatua ya nchi yake yaani Uingereza na Marekani ya kuanzisha vita huko Iraq licha ya nchi hizo kukosolewa pakubwa na nchi mbalimbali. Blair amedai kwamba, uamuzi wa kuishambulia Iraq ulikuwa sahihi na kwamba hali ya mambo ya Iraq ingekuwa mbaya zaidi kuliko hata ilivyo hivi sasa iwapo Saddam Hussein angeendelea kubakia madarakani. Vikosi vamizi vya Uingereza na Marekani viliishambulia Iraq mwaka 2003 na kumpindua madarakani Saddam Hussein kwa kisingizio kwamba nchi hiyo ilikuwa inamiliki silaha za maangamizi ya halaiki. Taasisi ya Iraq Body Count imetangaza kuwa, raia zaidi ya 112,000 pamoja na maelfu ya polisi na wanajeshi wa Iraq wameshauawa hadi hivi sasa tangu nchi hiyo ivamiwe kijeshi mwaka 2003.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO