Marekani imelazimika kusimamisha mpango wake wa ulinzi wa makombora barani Ulaya kwa kile ilichodai ni matatizo katika kupanua na kudhamini fedha zinazohitajika kwa ajili ya kukamilishia mpango huo. Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Chuck Hagel, amesema hayo mbele ya waandishi wa habari mjini Washington na kuongeza kuwa, Marekani imelazimika kusimamisha hatua ya nne na ya mwisho ya mfumo wa kujilinda na makombora wa nchi hiyo barani Ulaya unaojulikana kwa jina la APAA kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo ya kifedha.
Mradi wa Marekani wa kuweka kinga ya makombora hasa Ulaya Mashariki umekuwa ukilalamikiwa sana na Russia ambayo inalihesabu jambo hilo ni uchokozi wa wazi wa madola ya Magharibi dhidi ya ushawishi wa Russia katika eneo hilo. Hata hivyo Waziri wa Ulinzi wa Marekani hakusema kuwa nchi yake itaachana kikamilifu na mradi wake huo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO