Kundi la Boko Haram limetangaza kuwa limeteka nyara familia moja ya Kifaransa nchini Cameron na kuitahadharisha Paris juu ya kutumia nguvu kuwakomboa watu hao.
Taarifa ya kundi hilo kuhusiana na kutekwa nyara familia hiyo ya Kifaransa imetolewa kupitia mkanda wa video katika mtandao, sambamaba na ujumbe huo wa Boko Haram kwa maafisa wa Ufaransa. Kundi hilo aidha limesisitiza kuwa, iwapo Paris inataka kutumia nguvu za kijeshi kuwaokoa Wafaransa hao basi kundi hilo pia litatumia nguvu ili kujilinda.
Wafuasi wa kundi la Boko Haram Jumamosi ya Februari 19 waliwateka nyara Watalii 7 wa Kifaransa nchini Cameron karibu na mpaka wa nchi hiyo na Nigeria na kisha wakawahamishia nchini Nigeria.
Wakati huo huo raia mmoja wa Ufaransa aliyekuwa ametakwa nyara nchini Mali ameuawa. Mfaransa huyo anayejulikana kwa jina la Phillippe Verdo alitekwa nyara mwezi Novemba mwaka uliopita na taarifa zilizotolewa na msemaji wa al Qaida magharibi mwa Afrika AQIM zimeeleza kuwa, aliuawa Machi 10 katika kulipiza kisasi mashambulizi ya Ufaransa kaskazini mwa Mali.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO