Thursday, March 21, 2013

KOREA KASKAZINI YATISHIA KUSHAMBULIA VITUO VYA MAREKANI


Korea Kaskazini kwa mara nyingine imetishia kushambulia vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko nchini Japan na Guam na kusema kwamba itavilenga iwapo Washington itaendelea kurusha ndege zenye uwezo wa kubeba vichwa vya makombora ya nyuklia katika Penisula ya Korea.
Msemaji wa Jeshi la Korea Kaskazini amesema leo kuwa, Marekani inapaswa kutosahau kwamba zana zao za kijeshi zinaweza kufika katika kambi ya kijeshi ya Anderson huko Guam hadi nchini Japan ambako kuna maslahi ya Marekani.
Tahadhari hiyo imetolewa siku moja baada ya Pyongyang kulaani mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya Korea Kusini na Marekani kwenye eneo hilo na kusema kuwa ni ya kichokozi
Marekani imesema kuwa, ndege yenye uwezo wa kubeba vichwa vya makombora ya nyuklia ya B-52 imerushwa angani huko Korea Kusini katika manuva ya kijeshi ya hivi karibuni na kwamba hatua hiyo ni kwa ajili ya kusisitiza mshikamano wa Washington na Seol.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO