Sunday, March 10, 2013

CHAD YAJIUNGA NA KIKOSI CHA AFRIKA NCHINI MALI


Kikosi cha wanajeshi 2,000 wa Chad kilioko Mali ambacho kilitimiza dhima muhimu katika mapambano dhidi ya Waislamu wa itikadi kadi kimejiunga rasmi na kikosi cha Afrika kiliowekwa nchini Mali.
Mkuu wa majeshi wa Ivory Coast Soumaila Bakayoko ambayo nchi yake hivi sasa inashikilia uwenyekiti wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS amewaambia waandishi wa habari kwamba kuanzia leo hii ndugu zao wa Chad ambao wanapambana kuikomboa Mali wanajiunga na kikosi cha AFISMA.Amesema generali wa Chad atakuwa mmojawapo wa makamo wa rais wawili wa kikosi hicho cha Afrika.Vikosi vya Ufaransa viliingilia kati kijeshi kwa ghafla nchini Mali hapo tarehe 11 mwezi wa Januari katika juhudi za kuwazuwiya wapiganaji wenye mahusiano na Al Qaeda ambao walikuwa wakidhibiti eneo la kaskazini mwa Mali tokea mwezi wa Aprili mwaka 2012 kusonga kuelekea kusini mwa nchi hiyo na kuutishia mji mkuu wa Bamako.
Jumuiya ya ECOWAS imeahidiwa kupatiwa maelfu ya wanajehi kutoka nchi wanachama lakini vikosi vya AFISMA vimekuwa vikizorota katika kusaidia juhudi za Ufaransa kulikomboa eneo la kaskazini ya Mali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO