Waziri mkuu wa Tunisia, Ali Larayedh amesema kuwa amewasilisha orodha ya muundo wa serikali mpya ya Muungano, kwa rais Moncef Marzouki. Baraza jipya la mawaziri litaongozwa na chama cha Ennahda ,kikisaidiwa na vyama viwili vya kisiasa pamoja na wagombea wa kujitegemea. Ennahda kimeachia nyadhifa kadhaa za wizara ikiwemo wizara ya mambo ya nje , ulinzi na ile ya mambo ya ndani. Tunisia imekuwa ikikabiliwa na wakati mgumu tangu kutokea mauaji ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaid tarahe sita mwezi Februari. Mauaji yake yalisababisha ghasia na vurugu na hata kujiuzulu kwa serikali ya Muungano.
Muundo huo mpya utasalia kama ulivyo, hadi uchaguzi utakapofanyika kabla ya mwishoni mwa mwaka, alisema bwana Larayedh. Chama cha Ennahda kilishinda uchaguzi dhidi ya vyama vingine , lakini ushindi haukutosha kukiwezesha kuongoza peke yake. Tangu mwezi Julai mwaka jana, kimekuwa kikijaribu na kukosa kufaulu kupanua muungano wake kwa kujumuisha vyama vya upinzani ambavyo vimekikosoa kwa kujaribu kudhidbiti ulingo wa siasa Tunisia lakini kimekanusha madai hayo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO