Thursday, March 14, 2013

CHINA YATEUA RAIS MPYA


Kongresi ya Kitaifa ya Watu wa China imemeteua Xi Jinping, mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti, kuwa rais mpya wa nchi hiyo. Xi Jinping ameteuliwa kuwa rais wa China leo Alkhamisi baada ya kupigiwa kura na kongresi hiyo ya kitaifa mjini Beijing.
Uteuzi huo umekuja miezi mine baada ya mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 59 kuchukua uenyekiti wa chama tawala, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na rais anayeondoka Hu Jintao. Xi Jinping pia amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi ya China. Hu Jintao mwenye umri wa miaka 70 aliachia ngazi kama rais na kiongozi wa chama baada ya kushikilia nyadhifa hizo kwa muda wa takribani miaka 10.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO