Thursday, March 14, 2013

KAMANDA WA MAREKANI AWAONYA WANAJESHI WAKE AFGHANISTAN

Kamanda wa jeshi la Marekani nchini Afghanistan ameonya wanajeshi kwamba wanakabiliwa na ongezeko la kitisho cha mashambulizi kufuatia msururu wa kauli za uchochezi dhidi ya Marekani zilizofanywa na rais Hamid Karzai. Kikosi cha Kimataifa cha Kulinda Amani cha NATO - ISAF leo kimethibitisha maelezo yaliyomo kwenye waraka wa ushauri uliotumwa na Jenerali wa Marekani Joseph Dunford kwa makamanda wake wakuu. Jumapili iliyopita Karzai aliishutumu Marekani kwa kushirikiana na wanamgambo ili kuhalalisha kuwepo kwao nchini Afghanistan na akavipiga marufuku vikosi vyote vya kimtaifa dhidi ya kuingia katika vyuo vikuu kutokana na madai ambayo hayajathibitishwa ya kuteswa wanafunzi. Wanajeshi saba wa Marekani wamekufa Jumatatu wiki hii, ikiwa ni tukio baya kabisa kwa wanajeshi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO nchini Afghanistan hadi sasa kwa mwaka huu. Wanajeshi wawili wa Marekani waliuawa na wengine kumi kujeruhiwa katika shambulizi linalodaiwa kupangwa na mtu aliyekuwa amevaa sare ya jeshi la Afghanistan ambaye pia aliwauwa wanajeshi kadhaa wa Afghanistan.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO