Thursday, March 14, 2013

TUNISIA YAAPISHA SERIKALI MPYA


Rais Moncef Marzouki wa Tunisia amewaapisha Mawaziri wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa baada ya kupigiwa kura na kupitishwa na bunge la nchi hiyo. Waziri Mkuu wa Tunisia Ali Larayedh amesema Baraza lake la Mawaziri litahudumu hadi uchaguzi utakapofanyika mwaka ujao. Pia amewataka Watunisia kuwa wavumilivu na kuahidi kwamba serikali yake itafanya jitihada za kutatua matatizo ya kiuchumi na umasikini yanayowakabili.
Hayo yanajiri sambamba na kufariki dunia kijana wa Kitunisia Adel Khazri aliyejichoma moto katika kulalamikia hali mbaya ya maisha nchini humo.  Waziri Mkuu wa Tunisia amesema kuhusiana na tukio hilo kuwa, serikali yake imepata ujumbe uliokusudiwa na kwamba tukio hilo linasikitisha. Wananchi wengi wa Tunusia wanakabiliwa na hali mbaya ya kimaisha huku kiwango cha ukosefu wa ajira kikifikia asilimia 17 ambapo vijana wengi waliohitimu vyuo vikuu hawana kazi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO