Mahakama Kuu mjini Lilongwe, Malawi, imewaachilia huru washukiwa 11 wa kosa la uhaini akiwemo Peter Mutharika, kaka mdogo wa Rais Bingu wa Mutharika aliyefariki dunia mwaka uliopita.
Washukiwa hao ambao baadhi yao ni mawaziri wa zamani waliohudumu chini ya marehemu Bingu wa Muthaika, walikamatwa siku chache zilizopita kwa tuhuma za kumzuia Rais wa sasa, Joyce Banda kuchukua hatamu za uongozi baada ya kifo cha mtangulizi wake. Peter Mutharika anatuhumiwa kwamba alijaribu kulishawishi jeshi lichukue uongozi wa nchi ili Bi. Banda asiweze kutawala. Washukiwa hao wamekanusha mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana sambamba na kuwekewa masharti magumu.
Mahakama Kuu aidha imetwaa paspoti za washukiwa hao na kuwataka kutozungumzia kesi hiyo kwenye mikutano ya hadhara. Tangu alipochukua hatamu za uongozi mwaka jana nchini Malawi, Rais Joyce Banda amekuwa akitumia mkono wa chuma kuwanyamazisha wakosoaji wake.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO