Mjumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Fata-h ya Palestina katika Ukanda wa Gaza amesema, Rais Barack Obama wa Marekani katika safari yake kwenye eneo hilo hana ubunifu mpya wa kuwezesha kuanza tena mazungumo ya amani kati ya Palestina na Israel.
Yahya Rabah amesema, kinyume na ilivyotarajiwa Obama katika safari yake ya kutembelea ardhi za Palestina hana jipya la kuwezesha mazungumzo hayo yaliyosismama miaka kadhaa iliyopita yaanze tena. Mjumbe huyo wa harakati ya Fat-h ya Palestina ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unapaswa kuitambua serikali ya Palestina itakayoundwa kuanzia katika ardhi zilizoghusubiwa mwaka 1967.
Obama jana alianza safari yake ya siku 3 ya kutembelea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel, ikiwa ni ya kwanza baada ya kuchaguliwa tena kuiongoza Marekani. Amekutana na Waziri Mkuu wa Israel na anatarajiwa leo kukutana na Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO