Rais Barack Obama wa Marekani pamoja na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu kwa pamoja wamekariri misimamo ya kiadui dhidi ya Iran katika safari ya kwanza ya Obama huko Israel baada ya kuchaguliwa tena kuwa rais wa Marekani. Obama amesema Washington itafanya kila lililo muhimu kuizuia Iran isiwe na silaha za nyukli.
Obama pia amemuhakikishia Netanyahu kwamba serikali ya Marekani inashikamana na ahadi yake ya kuidhaminia usalama utawala wa Kizayuni wa Israel. Netanyahu kwa upande wake pia amemsifu Obama kwa kuitembelea Israel kwanza kabla ya nchi yoyote na kudai kuwa serikali yake inawanyooshea mikono ya amani na urafiki wananchi wa Palestina.
Safari ya siku 3 ya Obama huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel imepokelewa na maandamano ya Wapalestina huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO