Wednesday, March 20, 2013

HAKUNA MPANGO WA KUKUTANA NA OBAMA

Maafisa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas wamesema kuwa hakuna mpango wowote wa kufanyika mazungumzo kati ya viongozi wa harakati hiyo na Rais Barack Obama wa Marekani au manaibu wake katika safari atakayoifanya leo katika eneo. Usama Hamdan afisa wa Hamas anayehusika na masuala ya uhusiano wa kimataifa ambaye yuko Lebanon amesema kuwa safari ya Obama haina maslahi yoyote kwa Wapalestina bali inafanyika ili kuimarisha uungaji mkono wa Washington kwa utawala wa Kizayuni.  Aziz Duik spika wa bunge la Palestina na mmoja wa viongozi watajika wa Hamas pia ameishutumu Washington kwa kuendelea kupuuza matokeo ya mwenendo wa kidemokrasia huko Palestina na pia kuwapuuza wabunge halali wa Palestina. Washington imeiweka harakati ya Hamas katika orodha yake nyeusi na kuitaja harakati hiyo kama kundi la kigaidi. Rais Barack Obama leo anafanya ziara katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu katika hali ambayo Wapalestina wamefanya maandamano katika eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu  wakipinga safari yake hiyo.  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO