Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ramin Mehmanparasat amepinga madai ya Saudi Arabia kuhusu kuwepo raia wa Iran katika mtandao wa majasusi waliokamatwa hivi karibuni nchini humo.
Ramin Mehmanparast amekosoa vikali madai hayo ya maafisa wa Saudi Arabia na kusema madai hayo yamekuwa yakikaririwa mara kwa mara na hayana msingi wowote. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema madai hayo yasiyo na msingi yamesambazwa katika vyombo vya habari vya Saudia kwa lengo la kupotosha fikra za umma nchini humo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO