Marekani imetaka Jenerali muasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Bosco Ntaganda aliyeko katika ubalozi wa nchi hiyo nchini Rwanda apelekwe Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC).
Ntaganda alijisalimisha katika ubalozi wa Marekani Jumatatu iliyopita baada ya kuongoza uasi kwa kipindi cha miaka 15 huko Mashariki mwa Kongo. Pia aliomba kupelekewa katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC) ya The Hague. Jenerali Bosco Ntaganda anakabiliwa na mashtaka ya kutenda jinai za kivita na ukiukaji wa haki za binadamu aliofanyika kati ya mwaka 2002 na 2003 katika eneo la Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais Paul Kagame wa Rwanda alisema alipotembelea Umoja wa Mataifa hapo jana kwamba nchi yake itashirikiana na Ubalozi wa Marekani mjini Kigali ili kuhakikisha kwamba kesi ya Ntaganda inafanyika haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO