Rais wa Afghanistan Hamid Karzai na jeshi la kimataifa linaloongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya NATO wamefikia makubaliano ya kuondoka wanajeshi wa kigeni kutoka mkoa mmoja muhimu karibu na mji mkuu Kabul. Hata hivyo haijawa wazi ni lini Wanajeshi hao wa Marekani watakapoondoka eneo hilo. Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Afghanistan amesema kwamba jeshi la Marekani litaondoka mkoa wa Wardak katika siku chache zijazo, licha ya wasiwasi ya awali ya Marekani kwamba kuondoka kwao kungeacha pengo la ukosefu wa usalama. Taarifa ya Jeshi la Kimataifa la Kulinda Amani - ISAF nchini Afghanistan imesema kwamba wanajeshi wa Afghanistan watachukua majukumu ya kiusalama kutoka kwa wanajeshi wa ushirika katika jimbo la Wardak, lakini haikutaja hasa kuondoka kwa vikosi vya Marekani. Karzai kwa mara ya kwanza aliamuru kuondoka kwao mwezi uliopita baada ya wanavijiji kuwashutumu kwa kuwatesa na kuwauawa raia, madai ambayo wanajeshi wa Marekani waliyakanusha.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO