Msemaji wa Taliban nchini Afghanistan amesema kundi hilo limepata makombora ya masafa marefu aina ya Scari 20 na 30. Qari Yusuf Ahmadi amedai kwamba mnamo siku ya Jumatano wanamgambo wa Taliban walikishambulia kituo cha kijeshi cha vikosi vya kigeni katika eneo la Shur-ab mkoani Helmand kwa makombora 21 ya masafa marefu aina ya Scari 20 na 30. Hata hivyo Qari Ahmadi hakueleza ni vipi Taliban wameweza kupata makombora hayo. Shirika la Kijeshi la NATO lilitangaza kuwa shambulio la makombora lililofanywa na wanamgambo wa Taliban limesababisha hasara kubwa kwa kituo chake cha kijeshi huko Bastion katika mkoa wa Helmand. Kituo cha Bastion kilichoko kusini mwa Afghanistan ni moja ya vituo muhimu vya majeshi ya kigeni yaliyoko nchini humo na hadi sasa kimeshashambuliwa mara kadhaa na wanamgambo wa Taliban.
Wakati huohuo vikosi vya Australia vilivyomo kwenye muungano wa majeshi ya kigeni yanayoongozwa na Marekani yaliyoko nchini Afghanistan vimethibitisha kuwa vimewaua watoto wadogo wawili katika mkoa wa Uruzgan katikati mwa nchi hiyo
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO