Mahakama ya Stavropol nchini Russia imeanza kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Waislamu wa eneo la Stavropol wakitaka iondoshwe marufuku ya uvaaji wa hijabu kwenye shule za eneo hilo lililoko kusini mwa Russia. Wakili anayewatetea Waislamu hao Murad Mussayov amesema Waislamu wanapinga sheria iliyowekwa na Gavana wa jimbo hilo la kupiga marufuku uvaaji wa hijabu ya Kiislamu kwenye shule za jimbo hilo tokea mwanzoni mwa mwaka 2013.
Wakili Murad amekosoa vikali kusuasua kwa uendeshwaji wa kesi hiyo na kumtaka hakimu na waendesha mashtaka waharakishe mchakato wa kusikilizwa kesi hiyo. Kadhia hiyo ilipamba moto baada ya wanafunzi watatu wa Kiislamu waliovalia vazi la stara la hijabu kuzuiwa kuingia kwenye shule moja msimu wa joto uliopita, na suala hilo likatapakaa katika jamii ya wananchi wa Russia na hasa taasisi za Kiislamu na Waislamu kwa ujumla nchini humo.
Taarifa zinasema kuwa, kuna Waislamu wapatao laki tatu katika eneo la Stavropol kusini mwa Russia.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO