Saturday, March 23, 2013

WAISLAM 42 TOKEA MYANMAR WAUAWA


Kwa akali watu 42 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya moto kuteketeza kambi ya Waislamu wa Rohingya wa Myanmar waliokimbilia kaskazini mwa Thailand. Mae Hong Son Gavana wa jimbo la Narumol Paravat nchini Thailand amesema kuwa moto huo ulianza kuwaka jana Ijumaa na ulikuwa ukiendelea kuwaka kwa kasi ingawa vikosi vya kuzima moto vinaendelea kupambana na janga hilo.
Mamia ya Waislamu wa Myanmar kutoka kabila la Rohingya waliyakimbia makazi yao baada ya kuanza mapigano mapya yaliyoanzishwa na Mabudha wenye misimamo ya kufurutu mipaka dhidi ya Waislamu katika eneo la Meiktila, lililoko umbali wa kilomita 130 kaskazini mwa mji wa Naypyidaw. Kufuatia hali hiyo ya machafuko, Rais Thein Sein wa Mynmar alitangaza hali ya hatari katika mji wa Meiktila.
Inafaa kukumbusha hapa kuwa, serikali ya Mynmar inawabagua, inawatesa na kuwakandamiza Waislamu wa Rohingya wanaofikia idadi yao laki nane kwa madai kwamba, Waislamu hao ni wakimbizi waliokimbilia nchini humo wakitokea nchini Bangladesh.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO