Gazeti
la Washington Post limeripoti kuwa jeshi la Marekani limeandaa mipango kadhaa
ya kuishambulia kijeshi Syria ikiwemo kufanya mashambulio ya anga hadi kutuma
vikosi vya wanajeshi ndani ya ardhi ya nchi hiyo kwa madai ya kile kilichodaiwa
kuwa ni kudhibiti maeneo ya silaha za kemikali. Hata hivyo hadi sasa Washington
inashindwa kufanya hivyo kwa kuchelea upinzani wa kisiasa dhidi ya uvamizi wake
wa kijeshi na vilevile kukoesekana uratibu kati yake na nchi waitifaki katika
eneo. “Kama tungepaswa kufanya hivyo kesho ningesema kwamba hatuko tayari”
amesema afisa mmoja wa serikali ya Marekani ambaye hakutaka kutaja jina lake na
kuongeza kuwa kitu kimoja wanachojaribu kuepuka ni kuwa na kundi moja la
kulinda maeneo ya silaha za kemikali huku kundi jengine likishambulio maeneo
hayo kwa makombora. Kufuatia ripoti za shambulio la silaha za kemikali
lililofanywa karibu na mji wa Aleppo na makundi ya kigaidi nchini Syria
yanayofadhiliwa kijeshi na kifedha na nchi za kigeni zikiwemo za Magharibi na
za Kiarabu katika eneo, Rais Barack Obama wa Marekani alisema kuwa ameziagiza
timu maalumu kufanya uchunguzi makini ili kujua kama mstari huo mwekundu
umekiukwa au la. Ripoti zaidi zinaeleza kuwa serikali ya Obama inajaribu
kutumia kila njia ili kuibebesha serikali ya Syria lawama za shambulio hilo la
silaha za kemikali lililosababisha vifo vya raia kadhaa
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO