Wananchi wa Saudi Arabia wamefanya maandamano makubwa dhidi ya utawala wa Aal Saud katika miji mbalimbali ya nchi hiyo na kutaka Muhammad bin Nayef Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi hiyo ajiuzulu. Taarifa zinasema kuwa, wananchi wa Saudi Arabia wamefanya maandamano katika miji ya Riyadh, Makka, Madina, Qatif na Baridah wamefanya maandamano wakilalamikia kutiwa mbaroni na kuteswa wanawake wa nchi hiyo. Hali kadhalika idadi kadhaa ya wanawake katika miji ya Makka na Madina wamefanya maandamano wakisisitiza juu ya kufunguliwa mashtaka na kuhukumiwa wale wote waliohusika na jinai za kuwanyanyasa, kuwatesa na kuwadhalilisha wanawake waliotiwa mbaroni. Inafaa kuashiria hapa kuwa, wiki iliyopita kikosi cha usalama cha Saudi Arabia kiliwatia mbaroni karibu watu 300 katika mji wa Baridah katikati ya nchi hiyo, wengi kati yao wakiwa ni wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO