Sunday, March 03, 2013

NETANYAHU AFANYA KIKAO CHA SIRI NA MFALME WA JORDAN


Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ameripotiwa kufanya kikao cha siri na Mfalme Abdallah wa Pili wa Jordan  kuhusiana na kile kinachotajwa kuwa mwenendo wa amani wa Mashariki ya Kati. Duru za kidiplomasia zimeliarifu shirika la Habari la  Ufaransa la AFP  kuwa,  wiki iliyopita Netanyahu alisafiri hadi Jordan na kukutana na Mfalme Abdallah wa Pili ambapo walijadili mwenendo wa amani wa Mashariki ya Kati. Wawili hao pia walikutana mwezi Disemba kujalidi mgogoro wa Syria.
Hayo yanajiri huku mazungumzo kati ya Israel na Mamlaka ya Ndani ya Palestina yakiwa yamekwama tangu Septemba mwaka 2010, kutokana na siasa za Tel Avivi za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Palestina. Israel imeongeza ujenzi huo usio halali baada ya Palestina kuwa nchi mwanachama mwangalizi katika Umoja wa Mataifa tarehe 29 Novemba mwaka uliopita wa 2012.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO