Jeshi la Chad limetangaza kuwa askari wa nchi hiyo walioko nchini Mali wamemuua kiongozi wa waasi Mukhtar Belmokhtar. Jenerali Zacharia Gobongue msemaji wa jeshi la Chad ametangaza kuwa, jana Jumamosi mchana vikosi vya nchi hiyo vinavyopigana kaskazini mwa Mali viliharibu kikamilifu kambi ya wasi na kuwaua wapiganaji wa kadhaa wa waasi akiwemo kiongozi wao Mukhtar Belmukhtar.
Inasemekena kuwa, Belmukhtar aliyekuwa na miaka 40 ndiye aliamrisha mashambulizi ya mwezi Januari dhidi ya kiwanda cha gesi nchini Algeria yaliyopelekea zaidi ya watu 60 kuuawa. Kundi la Belmukhtar linajulikana kama "Batalioni iliyotia saini kwa damu" na lilijitenga na tawi la al Qaida Magharibi mwa Afrika (AQIM). Ijapokuwa taarifa ya kuuliwa kiongozi huyo wa waasi imetangazwa na televisheni ya Chad lakini hadi sasa duru nyingine binafsi hazijadhibitisha habari hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO