Waziri
Mkuu wa serikali halali iliyochaguliwa na wananchi huko Palestina amesema kuwa,
hatua ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwaua viongozi
wanamuqawama wa Palestina imeifanya harakati ya muqawama ya wananchi wa
Palestina kupata nguvu zaidi. Ismail Hania amesema hayo kwa mnasaba wa
kumbukumbu ya mwaka wa tisa tangu kuuawa shahidi Sheikh Ahmad Yassin aliyekuwa
kiongozi wa kiroho wa Hamas na kusisitiza kwamba, kuuawa viongozi mfano wa
Sheikh Ahmad Yassin, Abdul Azizi Rantissi na wengineo kumeufanya muqawama wa
wananchi wa Palestina uzidi kupata nguvu siku baada ya siku. Amesema,
Wazayuni walijihadaa kwa kudhani kwamba, kwa kuwaua viongozi wanamuqawama kama
Sheikh Ahmad Yassin wangeweza kung'oa mizizi ya muqawama na kuharibu misingi yake;
kwani hii leo muqawama wa Palestina una nguvu zaidi kuliko huko nyuma na
umekuwa ukipata wafuasi zaidi kila leo. Wakati huo huo, Harakati ya Mapambano
ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesisitiza kwamba, itaendelea na juhudi zake za
kutaka kuachiliwa mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya
kuogofya ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO