Rais wa Nigeria Good luck Jonathan amekataa pendekezo la kiongozi wa Kidini nchini humo la kutoa msamaha kwa wajumbe wa kundi lenye itikadi kali za kiislam la Boko Haram. Bwana Jonathan aliitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kwanza kama rais katika majimbo ya Borno na Yobe, ambayo yamekuwa yakikabiliwa na mashambulio ya kundi la Boko Haram. Tangu kuzuka kwa uasi wa kundi la Boko Haram mwaka 2009, eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria limekuwa kitovu cha ghasia za mauaji . Mamia ya watu wameuawa katika mashambulio kote katika jimbo hilo.
Sasa rais Goodluck Jonathan anafanya ziara yake ya kwanza katika majimbo ya Borno Yobe. Ataagiza kuanzishwa kwa miradi ya miundo mbinu huko , lakini pia atajaribu kujionea mwenyewe hali ya maeneo hayo yenye matatizo . Vikosi vya usalama vimefanya mashambulio kadhaa ya uvamizi kwenye maeneo yanayoshukiwa kuwa maficho ya wanamgambo hao, lakini havijafanikiwa kumaliza uasi huo.
Kiongozi mkuu wa kiislam Sultan wa Sokoto, alipendekeza kuwa msamaha kwa Boko haram utakuwa ni suluhu, lakini rais Jonathan amekataa pendekezo hilo, akisema wanamgambo hao sharti wasalimishe silaha na wajitambulishe . Rais Jonathan anajaribu kutumia ziara hii kuonyesha mamlaka yake dhidi ya tisho la usalama linaloongezeka , lakini anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kuchelewa kufanya ziara hiyo
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO