Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi zote duniani ziko huru kutuma meli za kivita katika maji ya kimataifa na kwa hivyo, manoari za Iran zimeamua kuelekea katika Bahari ya Atlantiki hivi karibuni. Admeli Habibullah Sayyari ameyasema hayo Alkhamisi mjini Tehran pembizoni mwa kongamano la 'Ulinzi wa Kitaifa, Ulinzi wa Pande Zote' na kuongeza kuwa, Msafara wa 24 wa Manoari za Jeshi la Wanamaji la Iran umeondoka Bandari ya Zhangjiagang nchini China. Msafara huo unaojumuisha manoari ya kurusha makombora ya Sablan na manoari ya Kharg yenye uwezo wa kubeba helikopta zilifika katika bandari hiyo ya China Jumatatu baada ya kusafiri umbali wa kilomita elfu 13 kwa muda wa siku 40. Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran amesema baada ya mafanikio ya katika Bahari ya Pasifiki sasa meli hizo za kivita za Iran zitaelekea Bahari ya Atlantiki. Katika miaka ya hivi karibuni Jeshi la Wanamaji la Iran limeimarisha harakati katika maji ya kimataifa kwa lengo la kulinda njia za bahari na kutoa ulinzi kwa meli za Iran zinazosheheni mafuta na za kibiashara. Shirika la Kimataifa la Usafiri Baharini IMO limelipongeza Jeshi la Wanamaji la Iran kwa mafanikio yake katika kupunguza uharamia katika eneo la Bahari ya Hindi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO