Rais Barack Obama wa Marekani ambaye anajitayarisha kwa ajili ya kuitembelea Israel amesema kuwa katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa utawala huo wa Kizayuni atafanya jitihada za kufikia mwafaka na Tel Aviv kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran.
Obama ambaye alikuwa akizungumza na televisheni ya Israel amesisitiza kuwa machaguo yote bado yako mezani na kwamba Marekani haitairuhusu Iran kumiliki silaha za nyuklia. Obama amedai kuwa Iran itakuwa na uwezo wa kutengeneza silaha za nyuklia katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
Matamshi hayo ya Rais wa Marekani ambayo yametolewa karibu wiki tatu kabla ya duru ya pili ya mazungumzo ya Iran na kundi la 5+1 huko Kazakhstan, yanaweza kuchunguzwa katika pande kadhaa.
Kwanza ni kuwa mienendo ya kisiasa ya Marekani hufuata malengo ya Wazayuni wa Israel dhidi ya Iran. Kwa maana kwamba daima Marekani hufanya jitihada za kuwaridhisha Wazayuni, suala ambalo halina mantiki yoyote.
Mara zote mazungumzo ya nyuklia Iran yanapofanyika katika anga chanya na yenye ishara za mafanikio viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel hutumia nyenzo zote kwa ajili ya kile wanachodai ni kuchafua sura ya Iran katika fikra za waliowengi duniani. Hususan ikitiliwa maanani ukweli kwamba matukio ya sasa ya Mashariki ya Kati yanaielekeza Israel katika changamoto nyingi.
Mazungumzo ya Iran na kundi la 5+1 linalojumuisha nchi za Marekani, Russia, Ufaransa, Uingereza, China na Ujerumani, huko Almaty nchini Kazakhstan yalifanyika katika anga ya kuridhisha ambapo Jamhuri ya Kiislamu ilitoa mapendekezo kamili ya kuondoa suutafahumu zilizopo. Hata hivyo ushahidi unaonesha kuwa, Marekani haitaki kuona suala hilo likitatuliwa na imekuwa ikitumia njia mbalimbali ikishirikiana na Israel kuhakikisha kwamba, mazumgumzo hayo yanafanyika katika anga isiyokuwa nzuri. Matamshi yanayotolewa na viongozi wa Israel na Marekani kuhusu miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia hapa nchini ni ushahidi wa ukweli huo.
Siku chache zilizopita Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alidai kuwa, hadi kufikia msimu ujao wa machipuo au kipindi cha joto kali cha mwaka huu Iran itakuwa imezalisha urani ya kutosha kwa ajili ya kutengeneza bomu la nyuklia. Netanyahu aliitaka jamii ya kimataifa iimewekee Iran mstari mwekundu katika shughuli zake za nyuklia.
Madai hayo yote yanatolewa katika hali ambayo utawala wa Kizayuni wa Israel unamiliki mabomu yasiyopungua miatatu ya nyuklia ambayo imeweza kuyatengeneza kwa msaada wa Marekani, Uingereza na Ufaransa. Kwa maneno mengine ni kuwa, mabomu ya nyuklia ya Israel si tishio kwa amani ya Mashriki ya Kati pekee bali usalama na amani ya dunia nzima.
Madai yaliyotolewa na Rais Barack Obama wa Marekani pia huenda yanataka kusema kuwa, kufeli kwa mazungumzo ya sasa ya Iran na kundi la 5+1 yumkini ukawa mwanzo wa vita vya Israel dhidi ya Iran. Hata hivyo ni wazi kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel hauna ujasiri wa kuishambulia kijeshi Iran kwani unatambua kuwa, kufanya ujinga kama huo na kushambulia taasisi za miradi ya nyuklia ya Iran kutakuwa na maana ya kutia saini hati ya kuangamizwa kwake. Kwa upande wake Marekani pia inatumia madai kama hayo dhidi ya Iran kwa ajili ya propaganda za vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na Wazayuni.
Ukweli wa mambo ni kuwa udiplomasia wa Marekani na Israel umejengeka juu ya msingi wa kukariri madai yasiyo na msingi wowote lengo lake likiwa ni kuzidisha mashinikizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutaka kuilazimisha Tehran ibadili misimamo yake mkabala wa malengo haramu ya Washington na Tel Aviv katika eneo la Mashariki ya Kati.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO